I made this widget at MyFlashFetish.com.

Thursday, August 5, 2010

UN YATOA PONGEZI KWA ZANZIBAR

UMOJA wa Mataifa umetoa pongezi zake kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Amani Abeid Karume na wananchi wote wa Zanzibar kwa kufanikisha kura ya maoni kwa amani na utulivu.

Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Dk. Asha-Rose Migiro aliyasema hayo wakati alipokuwa na mazungumzo na Rais Karume, Ikulu mjini Zanzibar.

Dk. Migiro, alimueleza Rais Karume kuwa Umoja wa Mtaifa umeridhika na hatua iliyofikiwa katika kufanikisha zoezi zima la kura ya maoni kwa amani, utulivu na mafanikio makubwa.

Akitoa salamu za Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bwana Ban Ki-moon, Dk. Migiro alieleza kuwa, UN imeridhishwa na makubaliano yaliyofanyika kati ya Rais Karume kupitia chama cha CCM na Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad kwa lengo la kuondosha kabisa migogoro iliyokuwepo hapo kabla.

Katika salamu hizo, Ban Ki-moon aliwatakia kila la heri wananchi wa Zanzibar katika kujenga amani na umoja ambao utawasaidia katika kufikia lengo lililokusudiwa ambapo UN itaendelea kutoa ushirikiano wake ili kuweza kupata mafanikio zaidi.

Katibu Mkuu huyo wa UN, aliipongeza Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa kuweza kusimamia vyema zoezi hilo kwa salama na amani.

Aidha, Dk. Migiro alimueleza Rais Karume kuwa UN imefarajika kwa namna Serikali anayoiongoza Rais Karume inavyotoa mashirikiano yake kwa Umoja huo sanjari na Mashirika yake yaliopo hapa Zanzibar.

Dk. Migiro alimueleza Rais Karume kuwa licha ya kumaliza muda wake wa Urais yeye mwenyewe binafsi pamoja na UN hautamsahau Rais Karume kwa juhudi zake kubwa alizozifanya katika uongozi wake ikiwa ni pamoja na kuwaletea wananchi wa Zanzibar maendeleo makubwa.

Sambamba na hayo, Dk. Migiro aliipongeza Zanzibar kwa kuendelea kuunga mkono Umoja wa Mataifa.

Nae Rais Karume alitoa shukurani zake kwa UN na kueleza kuwa mashirikiano mazuri yamekuwa yakipatika kutoka Umoja huo kupitia mashirika yake yaliopo nchini yakiongozwa na UNDP.

Rais Karume alieleza kuwa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar inajivunia mashirikiano na uhusiano mwema unaoupata kutoka Umoja wa Mataifa ambapo alieleza kuwa hata katika mafanikio yaliopatikana kwenye zoezi la kura ya maoni Shirika la Maendeleo la UNDP lilitoa ushirikiano wake mkubwa katika ufanikishaji.

Katika maelezo yake, Rais Karume alisema kuwa Umoja wa Mataifa umekuwa karibu sana na Zanzibar katika kutoa mashirikiano yake kwenye kuimarisha miradi ya maendeleo na uchumi.

Akieleza juu ya mafanikio yaliopatikana katika kura ya maoni, Rais Karume alisema kuwa mafanikio ya kura ya maoni kwa Wazanzibari wote kwani lengo na madhumuni ni kuimarisha umoja,mshikamano sanjari na amani na utulivu.

Sambamba na hayo, Rais Karume alimueleza Naibu Katibu Mkuu huyo wa UN kuwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa, inayokusudiwa kuundwa baada ya Uchaguzi Mkuu ujao ni ya wananchi wote wa Zanzibar.

Rais Karume alieleza kuwa Zanzibar imepata mafanikio kiuchumi, kisiasa na kijamii kutokana na mashirikiano mazuri yaliopo nchini, hivyo mafanikio hayo yataimarishwa zaidi kwa kukuza na kuimarisha umoja na mshikamano miongoni mwa Wazanzibari.

Rais Karume alisema kuwa wananchi wa Zanzibar wamepiga hatua kidemokrasia hali ambayo imeonekana kutokana na maamuzi na mapendekezo yao waliyoyatoa katika kuimarisha umoja na mshikamano.

Katika mazungumzo hayo, Rais Karume alimueleza Naibu Katibu Mkuu huyo kuwa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na wananchi wake wanaipongeza UN chini na uongozi wa Bwana Ban Ki-moon kwa mashirikiano mazuri na uhusiano mwema unaotoa kwa Zanzibar.

EU YAIPONGEZA ZANZIBAR KWA KURA YA MAONI

UMOJA wa nchi za Ulaya (EU) umetoa pongezi kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Amani Abeid Karume kutokana na kufanikisha zoezi la Kura ya Maoni na kueleza kuwa Zanzibar imepata maendeleo ya kupigiwa mfano kidemokrasia.

Mwakilishi wa Umoja wa nchi za Ulaya, Balozi Tim Clarke aliyasema hayo leo wakati alipokuwa na mazungumzo na Rais Karume Ikulu mjini Zanzibar.

Katika mazungumzo hayo ambapo Balozi Clarke akifuatana na baadhi ya Mabalozi wa nchi za Ulaya wanaofanyia kazi zao hapa Tanzania, alisema kuwa hatua iliyofikiwa Zanzib ar katika demokrasia ni kubwa na inapaswa kuungwa mkono.

Alisema kuwa Umoja wa nchi za Ulaya umeridhishwa na hatua hiyo na kutoa pongezi zake kwa Rais Karume pamoja na Wazanzibari wote kwa jumla kutokana na mafanikio makubwa waliyoyapata katika kuimarisha demokrasia.

Bwana Clarke na ujumbe wake walimueleza Rais Karume kuwa wanamatarajio makubwa kuwa Zanzibar itazidi kupiga hatua katika kuimarisha maendeleo yake sanjari na kudumisha umoja na mshikamano miongoni mwa wananchi wake hali ambayo itaipaisha Zanzibar katika medani na kiuchumi, kisiasa na kijamii.

Mwakilishi huyo, alimueleza Rais Karume kuwa ulimwengu mzima kwa namna zoezi hilo lilivyoendeshwa na hatimae kumalizika kwa ufanisi.

Katika mazungumzo hayo, viongozi hao walimueleza Rais Karume kuwa wameridhika na kuvutika kwa namna ya zoezi zima la Kura ya Maoni lilivyokwenda vizuri na kuwa ulimwengu mzima umefurahishwa na namna lilivyokwenda kwa amani na utulivu.

Walieleza kuwa EU itaendelea kutoa mashirikiano yake na Zanzibar kwa na kueleza kuwa wanamatumaini makubwa kuwa Umoja na mshikamano wa Wazanzibari utaendelea kuimarika zaidi.

Aidha, viongozi hao, walimueleza Rais Karume kuwa ni kiongozi anaependa umoja, mshikamano sanjari na kuimarishaji amani na utulivu hapa nchini kwa lengo la kuiletea Zanzibar maendeleo na maisha yenye utulivu.

Sambamba na hayo, viongozi hao waliwatakia Wazanzibari wote pamoja na viongozi wao wa kisiasa kuendelea kupata mafanikio katika kutekeleza umoja huo kwa lengo la kuleta maendeleo endelevu kwa wananchi na nchi yao kwa jumla.

Viongozi hao waliahidi kushirikiana bega kwa bega na Zanzibar katika kuhakikisha mafanikio zaidi yanapatikana katika kuimarisha sekta za maendeleo kutokana na kuthamini juhudi inazozichukua katika kufikia hatua hiyo..

Nae, Rais Karume kwa upande wake aliwaeleza viongozi hao wa EU kuwa zoezi la kura ya maoni ni la kihistoria ambalo limewapa wananchi wa Zanzibar haki ya kushiriki kikamilifu katika maamuzi wanayohisi yatawaletea manufaa zaidi.

Alieleza kuwa katika zoezi hilo la Kura ya Maoni hakuna alieshinda na aliyeshindwa kwani washindi ni Wazanzibari wote ambao wanapenda amani, umoja na mshikamano.

Rais Karume alieleza kuwa mafanikio ya zoezi hilo yamedhihirisha wazia kuwa Wazanzibari wamepevuka kisiasa.

Rais Karume alisema kuwa Wazanzibari wote wanapenda umoja, mshikamano sanjari na amani na utulivu na ndio maana wameunga mkono ili kutimiza na kuendeleza malengo yao hayo.

“Watu wote wa Zanzibar wanapenda amani”,alisema Rais Karume. Aidha, Rais Karume alisema kuwa kwenda vizuri kwa zoezi hilo kunatokana na taratibu nzuri zilizowekwa na Tume husika sanjari na wananchi wenyewe kuwa na mwamko na uwelewa juu ya zoezi hilo.

Katika mazungumzo hayo, Rais Karume alisema kuwa kufanikiwa kwa zoezi hilo kutatoa matokeo mazuri ambayo yataijenga Zanzibar mpya na yenye amani, umoja na mshikamano.

Rais Karume alitoa pongezi na shukurani kwa Washirika wa Maendeleo zikiwemo nchi za Umoja wa Ulaya kwa kuendelea kuiunga mkono Zanzibar katika kuimarisha sekta zake za maendeleo sanjari na kuunga mkono zoezi la Kura ya Maoni lililofanyika Julai 31 mwaka huu.

MAWAZIRI WATANO WA SMZ WATUPWA CHINI KWENYE KURA YA MAONI

Viongozi wandamizi wakuu watano wa serikali ya mapinduzi Zanzibari ni miongoni mwa wagombea waliokataliwa kugombea nafasi za uwakilishi katika uchaguzi mkuu kupita chama cha mapinduzi CCM.
Kwa mujibu wa matokeo ya kura hiyo iliyopigwa siku ya Jumapili waliokataliwa nafasi ya uwakilishi ni waziri wa Kilimo, Mifugo na Mazingira, Burhan Saadat Haji jimbo la Kikwajuni na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Sultani Mohammed Mugheiry jimbo la Mji Mkongwe.
Wengine ni naibu waziri wa kilimo Khatib Suleiman jimbo la Bububu, naibu waziri wa maji, ujenzi nishati na ardhi Tafana Kassim Mzee jimbo la Uzini na naibu waziri wa mawasiliano na uchukuzi, Mzee Ali Ussi jimbo la Chaani.
Nae mwenyekiti wa zamani wa umoja wa vijana wa CCM taifa Hamad Masauni aliekumbwa na kashfa ya kuhushi umri wake ameshinda kuwania nafasi ya ubunge jimbo la Kikwajuni, huku naibu katibu mkuu wa CCM Zanzibar Saleh Ramadhan Ferouz akiambulia nafasi ya tatu.
Hata hivyo mawaziri wengine akiwemo waziri Kiongozi, Shamsi Vuai Nahodha jimbo la Mwanakwerekwe na waziri wa elimu na mafunzo ya amali Haroun Suleiman Ali jimbo la Makunduchi wamechaguliwa tena kugombea nafasi ya uwakilishi.
Mawaziri wengine walioshinda katika kura hiyo ni Naibu waziri Kiongozi Ali Juma Shamuhuna jimbo la Donge, waziri wa Maji Ujenzi Nishati na Ardhi, Mansoor Yussuf Himid jimbo la Kiembesamaki na Waziri anaeshugulikia fedha na Uchumi Dk. Mwinyihaji Makame jimbo la Dimani.
Waziri wa Utalii Biashara na Uwekezaji, Samia Suluhu Hassan ameshinda nafasi ya Ubunge jimbo la Makunduchi, waziri wa mawasiliano na uchukuzi Machano Othman Said ameshinda nafasi ya uwakilishi jimbo la Chumbuni.
Aidha waziri wa nchi ofisi ya waziri kiongozi, Hamza Hassan Juma ameshinda nafasi ya uwakilishi jimbo la Kwamtipura.
Mawaziri wa Serikali ya Muungano wanaoendelea kutetea nafasi zao ni Dr. Hussen Mwinyi jimbo la Kwahani, naibu waziri wa mambo ya nje na ushirikiano Balozi Seif Ali Idd jimbo la Kitope na waziri anaeshughulikia masuala ya muungano Mohammed Seif Khatib jimbo la Uzini.
Katibu wa CCM wilaya ya Mjini Magharibi, Fatma Shomari amesema wagombea wengi walioshindwa katika kinyanganyiro hicho cha kura za maoni wamewasilisha malalamiko kwa kutoridhika jinsi ya

ZANZIBAR KUUNDA SERIKALI YA UMOJA WA KITAIFA

Wananchi wa Zanzibar wamekubali muundo mpya wa serikali ya umoja wa kitaifa baada ya uchaguzi mkuu wa Octoba mwaka huu kufuatia kupiga kura ya maoni ya ndio kwa asilimia 66.4 iliyofanyika jana.
Akitangaza matokeo hayo mwenyekiti wa tume ya uchaguzi Zanzibar Khatib Mwinyichande amesema wananchi waliopiga kura ya ndio ni laki moja, 88 elf, 705 sawa na asilimia 66.4.
Kura za hapana ni elfu 95, 613 sawa na asilimia 33.6, kura zilizoharibika ni elfu nane 721 sawa na asilimia 3.0 kati ya wananchi waliopiga kura laki mbili, elfu 93 na 36 sawa na asilimia 71.9.
Kwa mujibu wa matokeo hayo Mwinyichande amewatangaza wananchi waliopiga kura ya ndio wameshinda katika kura ya maoni kwa asilimia 66.4…

Akizungumza na wandishi wa habari mara baada ya kutolewa matokeo hayo hoteli ya Bwawani katibu mkuu wa CUF Seif Sharif Hamad amesema kura hiyo inaonesha wazanzibar wametaka kusahau yaliopita.
Amesema ushindi huo ni wa wazanzibari wote na kwamba matumaini yake ni kuanza ukurasa mpya kwa kuijenga Zanzibar mpya na kuwataka wananchi kushirikiana ili kuiletea maendeleo nchi yao….
Nae naibu katibu mkuu wa chama cha mapinduzi CCM Saleh Ramadhan Ferouz amesema matokeo hayo yametoa picha juu ya wazanzibari wanaotaka kuungana katika kuijenga Zanzibar.
Aidha amewataka wananchi kuufanya uchaguzi mkuu