Viongozi wandamizi wakuu watano wa serikali ya mapinduzi Zanzibari ni miongoni mwa wagombea waliokataliwa kugombea nafasi za uwakilishi katika uchaguzi mkuu kupita chama cha mapinduzi CCM.
Kwa mujibu wa matokeo ya kura hiyo iliyopigwa siku ya Jumapili waliokataliwa nafasi ya uwakilishi ni waziri wa Kilimo, Mifugo na Mazingira, Burhan Saadat Haji jimbo la Kikwajuni na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Sultani Mohammed Mugheiry jimbo la Mji Mkongwe.
Wengine ni naibu waziri wa kilimo Khatib Suleiman jimbo la Bububu, naibu waziri wa maji, ujenzi nishati na ardhi Tafana Kassim Mzee jimbo la Uzini na naibu waziri wa mawasiliano na uchukuzi, Mzee Ali Ussi jimbo la Chaani.
Nae mwenyekiti wa zamani wa umoja wa vijana wa CCM taifa Hamad Masauni aliekumbwa na kashfa ya kuhushi umri wake ameshinda kuwania nafasi ya ubunge jimbo la Kikwajuni, huku naibu katibu mkuu wa CCM Zanzibar Saleh Ramadhan Ferouz akiambulia nafasi ya tatu.
Hata hivyo mawaziri wengine akiwemo waziri Kiongozi, Shamsi Vuai Nahodha jimbo la Mwanakwerekwe na waziri wa elimu na mafunzo ya amali Haroun Suleiman Ali jimbo la Makunduchi wamechaguliwa tena kugombea nafasi ya uwakilishi.
Mawaziri wengine walioshinda katika kura hiyo ni Naibu waziri Kiongozi Ali Juma Shamuhuna jimbo la Donge, waziri wa Maji Ujenzi Nishati na Ardhi, Mansoor Yussuf Himid jimbo la Kiembesamaki na Waziri anaeshugulikia fedha na Uchumi Dk. Mwinyihaji Makame jimbo la Dimani.
Waziri wa Utalii Biashara na Uwekezaji, Samia Suluhu Hassan ameshinda nafasi ya Ubunge jimbo la Makunduchi, waziri wa mawasiliano na uchukuzi Machano Othman Said ameshinda nafasi ya uwakilishi jimbo la Chumbuni.
Aidha waziri wa nchi ofisi ya waziri kiongozi, Hamza Hassan Juma ameshinda nafasi ya uwakilishi jimbo la Kwamtipura.
Mawaziri wa Serikali ya Muungano wanaoendelea kutetea nafasi zao ni Dr. Hussen Mwinyi jimbo la Kwahani, naibu waziri wa mambo ya nje na ushirikiano Balozi Seif Ali Idd jimbo la Kitope na waziri anaeshughulikia masuala ya muungano Mohammed Seif Khatib jimbo la Uzini.
Katibu wa CCM wilaya ya Mjini Magharibi, Fatma Shomari amesema wagombea wengi walioshindwa katika kinyanganyiro hicho cha kura za maoni wamewasilisha malalamiko kwa kutoridhika jinsi ya
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment