I made this widget at MyFlashFetish.com.

Monday, November 1, 2010

WAKATI WOWOTE KUTOKA SASA TUTAPATA KUMJUA RAIS MPYA WA ZNZ

Umati mkubwa wananchi umekusanyika mbele ya kituo cha kutangazia matokeo ya uchaguzi katika hoteli ya Bwawani wakiisindikiza tume ya uchaguzi Zanzibar (ZEC) kutangaza matokeo ya uchaguzi huo uliofanyika juzi yatolewe haraka badala ya kutangazwa kwa utaratibu wa kusuasua.

Wananchi hao walijaa ndani ya hoteli na ukumbi wa salama wa hoteli hiyo huku baadhi yao wakiwa nje ya geti ambapo jeshi la polisi lililazimika kufunga lango na kuwazuwia baadhi yao wasiingie ndani kutokana na kuwa ndani ya hoteli hiyo kulijaa umati mkubwa wa watu .

Vijana na akina mama walikuwa wengi katika lango la hoteli hilo huku wakiimba na nyimbo huzuni na kusoma quran tukufu na kumshitakia Mwneyenzi Mungu kwa kuomba dua za kumhifadhi Maalim Seif na balaa na kuitakia kheri Zanzibar na watu wake katika kipindi hiki cha utangazaji wa matokeo.

Jeshi la polisi jana lilionekana likifanya kazi kubwa na kuhakikisha usalama unapatikana katika eneo lote la hoteli hiyo ikiwa pamoja na kuwasogeza wafuasi hao wakiwataka wakae chini huku magari ya maji ya kemikali na polisi waliovalia kivita wakiwa pembeni kwa wafuasi hao.

Wakizungumza na waandishi wa habari wananchi hao wamesema hawataandoka maeneo hayo hadi hapo tume ya uchaguzi itakapotangaza matokeo ya urais kwani imekuwa ukichelewesha kwa makusudi na kuishutumu tume hiyo kwamba inataka kubadilisha matokeo halisi yaliokusanywa vituoni.

“Hapa hatutaondoka mpaka tusikie rais akitajwa maana huu ni uchaguzi wane unafanyika nchini kwetu lakini imekuwa kawaida kukawilishwa matokeo lakini sisi tunachotaka ni kutangazwa kwa matokeo na sio jambo jengine” alisema Asha Abdallah ambaye ni miongoni mwa akina mama waliokuja na watoto wake.

Wananchi hao ambao wengi wao wanaonekana ni wafuasi wa chama cha wananchi (CUF) wamesema wasingependa kufanya fujo wala kusababisha madhara kwa mwengine lakini kwa kuwa wanataka maoni yao yaheshimiwe hawana budi kutetea haki yao ambayo imekuwa ikiporwa kwa muda mrefu na watawala.

“Mtatusamehe sana waandishi wa habari na waangalizi sisi tumekuja hapa sio lengo letu kufanya fujo lakini lengo letu ni kuwa mawazo yetu na maamuzi yetu tulioamua ndani ya kisanduku cha kura tunataka yaheshimiwe na watawala kwa hivyo tunataka ushindi wa maalim seif apewe mwenyewe haraka..tunachotaka maalim seif atangazwe maana matokeo yanaonesha yeye anaongoza akifuatiwa na Dk Shein” alisema Hassan Hamad Nassor.

Tokea juzi tume ya uchaguzi Zanzibar kupitia mwenyekiti wake, Khatib Mwinyichande imekuwa ikitoa matokeo ya urais huku matokeo ya uwakilishi, udiwani na ubunge yakitolewa majimboni.

Kwa mujibu wa Khatib hadi sasa CUF imepata majimbo matatu kwa upande wa Unguja ikiwemo jimbo la Mji Mkongwe, Magogoni na Mtoni huku majimbo mengine mengi yaliotangazwa yakishikiliza na CCM ikiwemo la Donge na Uzini ambayo yameshinda kwa zaidi ya asilimia 90

No comments:

Post a Comment