I made this widget at MyFlashFetish.com.

Monday, November 1, 2010

KAZI ZA KUHESABU KURA ZA RAIS WA TANZANIA ZINAENDELEA KUHESABIA

Kazi za kuhesabu kura kwa ajili uchaguzi wa urais wa jamhuri ya muungano Tanzania zinaendelea katika maeneo mbali mbali hasa yale ya Tanzania bara.

Hata hivyo baadhi ya maeneo ya Zanzibar kazi za kuhesabu kura zimalizika na kinachosubiriwa ni kutangazwa kwa matokeo ya jumla ya tume ya taifa ya uchaguzi NEC.

Waangalizi wa kimataifa wamesema kazi za upigaji kura zilifanyika kwa amani na utulivu licha ya kujitokeza kasoro ndogo ndogo.

Mkurugenzi wa tume ya taifa ya uchaguzi NEC Rajab Kiravu amesema uchaguzi wa majimbo yakiwemo majimbo manne ya Zanzibar umeahirishwa kutokana na upungufu wa karatasi za kupigia kura.

Amesema uchaguzi huo utarejewa tena Novemba 14 mwaka huu

No comments:

Post a Comment